emblem
OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
WAKALA YA BARABARA ZA VIJIJINI NA MIJINI

TARURA

MIRADI YA BIL. 2.55 BARABARA ZA LAMI YAPITIWA NA MBIO ZA MWENGE KAGERA


MIRADI YA BIL. 2.55 BARABARA ZA LAMI YAPITIWA NA MBIO ZA MWENGE KAGERA


Kagera


Miradi 8 ya barabara za lami zenye urefu wa Km 5.2 yenye thamani ya shilingi bilioni 2.5 zimepitiwa na mbio za Mwenge wa Uhuru katika halmashauri 8 mkoani Kagera.


Meneja wa TARURA Mkoa wa Kagera, Mhandisi Wilson Charles amesema kuwa barabara za lami zilizopitiwa na mwenge wa uhuru ni miongoni mwa Km 8 zilizokamilika kwa mwaka 2023/2024.


Amesema miradi hiyo imeweza kuwaondolea adha ya usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa halmashauri hizo kwani barabara hizo zimejengwa maeneo ya kutolea huduma za kijamii ikiwemo shule, zahanati, vituo vya afya, hospitali, viwandani pamoja na kwenye makazi ya watu.


“Barabara hizi zimekuwa na maana sana katika kuboresha huduma kwa wananchi ambapo awali hakukuwa na barabara na hivyo kusababisha wananchi kushindwa kupita na kupata huduma za kijamii kwa wakati kwa sababu ya barabara”.


"Barabara za Lami zimeongeza mabadiliko makubwa sana katika swala la kuongeza hadhi na kukuza miji na vijiji, tunasimamia vizuri wakandarasi na vijiji vinaendelea kupata lami, wananchi wanapata taa za barabarani na kukuza uchumi wao na sisi hatutachoka tutaendelea kutekeleza kwa weledi mkubwa", ameongeza.


Mkoa wa Kagera una mtandao wa barabara zinazohudumiwa na TARURA zenye urefu wa kilometa 6,403 na kati ya hizo kilometa 132.2 tayari zina lami na mwaka 2024/2025 TARURA imepanga kujenga barabara za lami Km 8.