emblem
OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
WAKALA YA BARABARA ZA VIJIJINI NA MIJINI

TARURA

IJUE TARURA


Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA) ulianzishwa chini ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kupitia Sheria ya Uanzishaji Wakala wa Serikali, Sura 245. Uanzishwaji wa Wakala huu ulitangazwa kwenye Gazeti la Serikali Namba 211 la tarehe 12 Mei, 2017 na kuanza kutekeleza majukumu yake rasmi ya kusimamia ujenzi na matengenezo ya mtandao wa barabara za Vijijini na Mijini zenye urefu wa Kilometa 108,946.19 mwezi Julai, 2017. Uanzishwaji wa TARURA ni kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 kama ilivyoainishwa kwenye Ibara ya 39(iii).