emblem
OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
WAKALA YA BARABARA ZA VIJIJINI NA MIJINI

TARURA

TARURA KUSHIRIKIANA NA ESRF KUFANYA UTAFITI NA TATHMINI YA MCHANGO WA UBORESHAJI WA BARABARA ZA VIJIJINI


TARURA KUSHIRIKIANA NA ESRF KUFANYA UTAFITI NA TATHMINI YA MCHANGO WA UBORESHAJI WA BARABARA ZA VIJIJINI


Dar Es Salaam


Wakala ya Barabara za Vijiiini na Mijini (TARURA) kwa kushirikiana na Taasisi ya utafiti wa Kiuchumi na Kijamii ( ESRF) zimeanza maandalizi ya kufanya utafiti ili kubaini mchango wa TARURA katika kuboresha uchumi wa jamii kutokana na miradi inayotekelezwa.


Utafiti huo unaotarajiwa kusimamiwa na ESRF utahusisha mikoa 8 ikiwemo Kilimanjaro, Iringa, Pwani, Simiyu, Kagera, Katavi, Morogoro na Dodoma ili kubaini mchango wa Wakala katika uchumi wa wananchi tangu kuanzishwa kwake mwaka 2017.


Akizungumza wakati wa mafunzo maalum kwa wataalam watakaoshiriki utafiti huo, Mkurugenzi Mkuu wa ESRF Prof. Fortunata Makene amewataka wataalam hao kuzingatia mafunzo yanayotolewa ili kuhakikisha utafiti utakaofanyika uwe na tija kwa taasisi hizo na serikali kwa ujumla.


"Mafunzo haya myazingatie kwa umakini wa hali ya juu ili mkawe mabalozi wazuri wa ESRF na TARURA na mwisho wa siku tupate majibu yaliyozingatia utaalam na vigezo vyote vya tafiti", amesema Prof. Makene


Akitoa Salam za Mtendajj Mkuu, Mchumi Mwandamizi kutoka TARURA Bw. Ally Ismail alisema mafuzo haya ni hatua muhimu katika kuhakikisha zinapatikana takwimu sahihi na za kuaminika, ambazo zitasaidia katika kuboresha miundombinu ya Barabara za wilaya zinazotekelezwa na TARURA.